Rais wa DICOTA, Dkt Frank Minja akiwa na Mhe Balozi Liberata Mulamula, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, jijini Dodoma, leo Aprili 22, 2021.
Salaam za Diaspora waishio Marekani zilipokelewa vizuri mno na Mhe Waziri Mulamula pamoja na Timu yake, huku wakiahidi kushirikiana nasi kutatua kero zetu, pamoja na kutuhamasisha tuzidi kuchangia maendeleo ya Taifa letu, hususan kwa kurudisha utaalamu wetu nyumbani (skills transfer).
Tulijadili pia mahitaji muhimu na vipaumbele kwa Diaspora waishio Marekani, pamoja na msimamo rasmi wa DICOTA kuhusu mchakato wa uraia pacha (Dual citizenship) vs. hadhi maalum (Special Status).